KUTOKA MOROCCO: Mkuu wa msafara Yanga SC, Rogers Gumbo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa timu hiyo amesema maandalizi kuelekea mchezo wa hapo kesho dhidi ya AS FAR yanaendelea vizuri.
Gumbo amesema wanasubiri siku ya mchezo ifike kwa kuwa wamejiandaa vyema licha ya hali ya hewa kubadilikabadilika kila mara, amesema tokea wafike Morocco hawajakumbana na changamoto yoyote kutoka kwa wenyeji wao.
#CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika