Marekani imetangaza vikwazo vipya vya kupunguza mauzo ya mafuta ya Iran, vikwazo hivi vinalenga meli 14. Haya yanajri muda mfupi tu baada ya nchi nchi hizo mbili kuhitimisha mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja nchini Oman.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Tommy Pigott, alisema siku ya Ijumaa kwamba Iran inatumia mapato ya mafuta yake “kufadhili shughuli za kuleta taharuki duniani na kuongeza ukandamizaji ndani ya Iran.”

Pigott alisema katika taarifa: “Rais Donald Trump ameahidi kupunguza mauzo haramu ya mafuta na bidhaa za kemikali zitokanazo na mafuta za utawala wa Iran, katika hatua ya kuishinikiza utawala huu.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema itazuia miamala yoyote na meli 14 zinazodaiwa kutumika kusafirisha mafuta ya Iran.

Pia ilitangaza vikwazo dhidi ya mashirika 15 na watu wawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *