Nchimbi awakumbusha viongozi wa dini wajibu kuombea taifaNchimbi awakumbusha viongozi wa dini wajibu kuombea taifa

MAKAMU wa Rais, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema viongozi wa dini wana wajibu wa pekee wa kuliombea taifa kama ambavyo Biblia Takatifu ilivyoelekeza.

Dk Nchimbi aliyasema hayo wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC) iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church uliopo Mbezi Jogoo, Dar es Salaam juzi.

Aliwahimiza kuendelea kumuombea afya njema, busara na hekima Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ndiye kiongozi mkuu wa nchi na kupitia yeye nchi itaendelea kuwa salama. Aliwataka viongozi hao kutambua wanapaswa kutimiza wajibu na kuwa na moyo wa utumishi kwa nchi, waumini na kanisa kwa ujumla.

Aidha, Dk Nchimbi aliwahimiza viongozi wa dini kutambua wajibu wa kulinda mazingira kwa kuendeleza jitihada za uhifadhi mazingira na kuwafundisha waumini kujiepusha na ukataji miti, uchomaji misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji.

Aliwasihi kutoa mafundisho yatakayochagiza upandaji miti mipya kwa wingi kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo. Katika hafla hiyo, Dk Nchimbi alisema pamoja na utoaji wa eneo la ekari 12 mkoani Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya Baraza la CPTC, pia Rais Samia alitoa Sh milioni 100 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi huo. Alisema rais aliunda wizara maalumu kusimamia mahusiano ambayo imeendeleza ushirikiano baina ya serikali na taasisi za dini.

Alizishukuru taasisi za dini kwa mchango wanaotoa katika huduma za kijamii kama vile shule na huduma za afya pamoja na malezi ya watoto. Aliwaomba viongozi hao wa dini kusimamia maadili ya nchi kwa kujenga taifa la watu wanaoheshimu na wanaojali uwepo wa Mungu.

Vilevile kujenga taifa la watu waaminifu, wanaoheshimiana, wanaopenda nchi, kushirikiana na kuepusha taifa la watu wabinafsi na wapenda rushwa. Pia, Dk Nchimbi alisema serikali itaendelea kusimamia amani ya nchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *