
Uamuzi huu, hatua ya kwanza madhubuti iliyochukuliwa na Algiers dhidi ya Abu Dhabi, unakuja huku kukiwa na mashambulizi yaliyofichwa yaliyoanzishwa na Algeria dhidi ya Falme za Kiarabu kwa miaka kadhaa. Suala linalojadiliwa, haswa, ni kuongezeka kwa ushiriki wa taifa la Ghuba katika masuala ya kikanda, ambayo yanaonekana kwa mashaka na mamlaka ya Algeria.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mgogoro unaibuka kati ya Algiers na Abu Dhabi. Katika hatua yake ya kwanza thabiti dhidi ya Falme za Kiarabu (UAE), Algeria imesitisha makubaliano yake ya kwanza ya huduma za anga za nchi mbili na taifa hili la Ghuba. Mkataba huu unasimamia safari za ndege kupita katika maeneo yao, unaondoa vikwazo vya uagizaji na ushuru wa forodha kwa baadhi ya bidhaa, na, muhimu zaidi, unadhibiti safari za ndege kati ya nchi hizo mbili. Kwa kifupi: Uamuzi wa Algiers unamaanisha, miongoni mwa mambo mengine, kusitishwa kwa safari za ndege kati yao. Tofauti na hali ya sasa, mashirika ya ndege ya Air Algérie na Imarati hivi karibuni hayataweza tena kutoa safari za ndege kati ya Algiers na Dubai, kwa mfano.
Ingawa mamlaka ya Algeria haijatoa maelezo yoyote kwa hatua hii, hata hivyo ni sehemu ya mashambulizi yaliyofichwa ambayo Algiers imeyaanzisha dhidi ya Falme za Kiarabu katika miaka ya hivi karibuni, bila kuyataja moja kwa moja.
Sababu: Kuingilia masuala mbalimbali ya ndani ya nchi kunakoongezeka kwa Abu Dhabi kama vile Libya, Sudan, na Sahel, ahali ambayo imekuwa ikichochea chuki na hasira huko Algiers, ambapo Imarati inashutumiwa kuchochea ukosefu wa utulivu wa kikanda. Mwezi Oktoba mwaka uliyopita, rais wa Algeria alilaani vitendo vya “nchi ndugu” bila kuiita jina, lakini hakuna shaka kwamba Abdelmadjid Tebboune alikuwa akiilenga Imarati.
Ingawa mashambulizi hayo yalikuwa yamefichwa hadi sasa, nchi hizi mbili zinaonekana kupaza sauti.