Dunia imepigwa na butwaa baada ya wizara ya sheria ya Marekani kuweka wazi nyaraka za Epstein, mhalifu wa ngono na mwanamtandao mkubwa wa mambo machafu na ya giza.
Jina lake halisi ni Jeffrey Epstein, raia wa Marekani mwenye asili ya uyahudi, bilionea mkubwa sana aliyetengeneza mtandao mkubwa wa mawasiliano na watu wakubwa na maarufu duniani kwenye nyanja zote.
Viongozi wakubwa wa kisiasa, wa kidini, wa michezo na hata wafanyabiashara, walikuwa kwenye orodha yake. Alimiliki kisiwa chake binafsi na kujenga majumba yake ya kifahari kwa ajili ya starehe.
Huko aliandaa tafrija mbalimbali zilizojaa kila aina ya ushetani, ikiwemo ngono kwa watoto wa wadogo, kula nyama za watu na kunywa damu, hatari sana!
Mhalifu wa ngono na mwanamtandao mkubwa wa mambo machafu na ya giza, Jeffrey Epstein. Picha na Mtandao
Alikamatwa kwanza mara ya kwanza mwaka 2005, kufuatia uchunguzi uliofanywa na polisi wa Palm Beach huko Florida kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya kabinti ka miaka 14.
Baba wa kabinti ndiye aliyeripoti polisi, na baada ya uchunguzi ikabainika kuna mabinti wengine 36 walinyanyaswa. Kesi ikaenda hadi 2008 alipokutwa na hatia. Akakaa nguvuni kwa miaka 13, na kuachiwa.
Akakamatwa tena Julai 2019 kwa tuhuma za usafirishaji haramu wa watoto kwa ajili ya kuwatumia kingono.
Akiwa jela, akajiua Agosti 10, 2019. Japo wapembuzi wa mambo wanasema aliuawa ili kupoteza ushahidi kwa sababu angewataja wengi katika mhandao wake.
Hata hivyo wapigania haki walipiga kelele nyingi kutaka taarifa zaidi kumhusu zitolewe ili mtandao wake ujulikane kwa sababu haiwezekani akafanya yote hayo peke yake.
Baada ya mashinikizo mengi, ndipo Januari 2026 wizara ya sheria ya Marekani ikakusanya nyaraka zaidi ya milioni tatu zinazomhusu, na kuziweka hadharani.
Nyaraka hizi ni kutoka kwenye mawasiliano aliyowahi kuyafanya na watu mbalimbali, picha na video zake.
Hapo ndipo watu wengi maarufu wakabainika kuwa walikuwa karibu sana na Epstein wakiwasiliana kupanga mambo mbalimbali.
Kwa kuwa sisi ni wanamichezo, tuangalie ulimwengu wetu ulivyoguswa na nyaraka hizi.
Mwekezaji wa klabu ya Crystal Palace ya Uingereza, Josh Harris. Picha na Mtandao
JOSH HARRIS
Mwekezaji wa klabu ya Crystal Palace ya Uingereza, Josh Harris, ametajwa na NYARAKA kama mtu aliyeendelea kufanya mawasiliano na Epstein kwa barua pepe na simu kwa miaka mingi licha ya kukutwa na hatia.
Harris ni mmiliki wa kampuni ya Apollo Global Management ambayo inamiliki timu za michezo mbalimbali kama mpira wa kikapu – NBA- (Philadelphia 76ers), mpira wa magongo – NHL- (New Jersey Devils), na soka la kimarekani – NFL- (Washington Commanders).
Mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly. Picha na Mtandao
TODD BOEHLY
Mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly, amenaswa na NYARAKA hizo kupitia mawasiliano yake ya barua pepe kwa Epstein na kufanya mikutano kadhaa.
Nyaraka zinaonesha kwamba mwaka 2011 Epstein ndiye aliyetaka kuunganishwa na Boehly ambaye wakati huo alikuwa mmiliki mwenza wa timu ya baseball ya Los Angeles Dodgers, na mshirika wa kampuni ya usimamizi wa wanamichezo ya Guggenheim Partners.
Mwanahisa mkubwa wa klabu ya Celtic ya Scottland, Dermot Desmond. Picha na Mtandao
DEEMINT DESMOND
Mwanahisa mkubwa wa klabu ya Celtic ya Scottland, Dermot Desmond, naye ametajwa kwenye nyaraka hizo kama mtu aliyekuwa na mawasiliano ya karibu na Epstein.
Desmond ametajwa kupitia barua pepe zilizoandikwa kwa Epstein mwaka 2010, kwa niaba ya tajiri mmoja aliyekuwa akimiliki uwanja wa golf, Gerald G Barton.
Kwenye jumbe hizo, Epstein aliambiwa na mtu aliyeandika barua pepe kwa niaba ya Barton kwamba kuna bilionea raia wa Ireland anayeitwa Desmond – mmiliki wa uwanja wa golf – yuko tayari kutoa mamilioni ya dola kusaidia kuukuza mchezo wa golf.
KUTAJWA SIO HATIA
Hao ni baadhi ya wengi waliotajwa kwenye nyaraka za Epstein.
Kutajwa pekee sio hatua, ni kama inavyosema sheria namba 11 ya mpira wa miguu.
Sheria hii inayohusu kuotea inasema kuwa kwenye eneo la kuotea sio kosa.
Kosa ni kubusika na mchezo, au kuingilia mchezo.
Na ndivyo ilivyo kwa nyaraka za Epstein. Kutajwa pekee sio kosa…umetajwa ukihusika na nini, ndio kosa.
Wapo waliotajwa wakihusika na nyama mbalimbali za biashara haramu, mapinduzi ya kisiasa na hata biashara haramu.
Wapo waliotajwa katika zile tafrija za kishetani na mambo mengine mengi sana.
Hakuna mtanzania aliyetajwa moja kwa moja, lakini Tanzania kama nchi imetajwa kuhusika kama njia ya kupitishia watoto kutoka Somalia na Kenya wanauzwa katika biashara haramu ya usafirishaji watu.
Hawa ni miongoni mwa watoto waliotumika aidha kwenye ngono au makafara…inasikitisha sana!