• Kiongozi wa ODM na Seneta wa Siaya, Oburu Oginga, amefafanua kuwa chama hicho kinalenga wadhifa wa Naibu Rais katika mazungumzo yanayoweza kufanyika na chama cha UDA cha Rais William Ruto
  • Alisema matamshi yake ya awali yalitafsiriwa vibaya na kusisitiza kuwa chama hakina uhasama wa kibinafsi na Naibu Rais Kithure Kindiki
  • Oburu alisisitiza kuwa ODM inatafuta mgao wake wa nyadhifa za kuchaguliwa kulingana na mamlaka ya wananchi, si kwa misingi ya uhasama wa watu binafsi

Kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Oburu Oginga ameeleza bayana dhamira ya chama hicho katika mazungumzo na United Democratic Alliance (UDA) ya Rais William Ruto.Alliance (UDA).

Kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Oburu Oginga
Kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Oburu Oginga alisema matamshi yake ya awali kuhusu kiti cha DP yalitafsiriwa vibaya. Picha: Oburu Oginga.
Source: Twitter

Kauli za hivi karibuni za seneta huyo wa Siaya zinaonyesha mabadiliko makubwa kutoka matamshi yake ya awali huko Kisumu, ambapo alipendekeza kuwa ODM haikuwa na mpango wa kuwania wadhifa wa Naibu Rais katika muungano unaowezekana na Kenya Kwanza.

Katika hafla ya utoaji wa fedha za Nyota Capital iliyofanyika Kisumu Jumatatu, Februari 2, Oburu aliwasilisha ushiriki wa ODM kama unaoongozwa na maslahi ya kitaifa badala ya tamaa za kibinafsi.

Pia soma

Oburu Oginga adokeza kuhusu lini ODM watamtema Ruto ili kuwa na mgombea urais wao 2027

Alisisitiza kuwa chama cha Machungwa kingejadiliana kwa ajili ya mgao wake wa haki bila kulenga nyadhifa za viongozi waliopo madarakani.

Alieleza kuwa chama hicho kinamilikiwa na Wakenya wote, si watu wa Luo Nyanza pekee, akibainisha kuwa tayari kinaongoza wizara muhimu kama Hazina na Nishati.

Je, ODM inalenga kiti cha Kindiki?

Hata hivyo, akizungumza Mombasa Jumatano, Februari 11, Oburu alisisitiza kuwa kauli zake za awali zilieleweka vibaya.

Akiwa ameshangiliwa na wanachama wa ODM, mwanasiasa huyo mkongwe alifafanua kuwa chama hicho kwa hakika kinalenga wadhifa wa Naibu Rais.

Oburu alieleza kuwa alimaanisha tu kwamba ODM haina tatizo la kibinafsi na mwenye kiti cha sasa, Naibu Rais Kithure Kindiki.

“Kuna jambo jingine ambalo watu wengine walilitafsiri vibaya. Walisema nilidai hatutaki nafasi ya Naibu Rais. Nafasi hiyo ya Naibu Rais ndiyo hasa tunayolenga, ndiyo tunayoikusudia. Nilichosema ni kwamba hatuna uhasama wa kibinafsi na Naibu Rais huyo; binafsi hatuna tatizo naye. Lakini nafasi hiyo ni ya umma na ya kuchaguliwa iwapo uchaguzi utafanyika,” Oburu alisema, akishangiliwa na wanachama wa ODM hukoMombasa.

Kwa nini Oburu alimkosoa Uhuru?

Pia soma

Ruto amkemea Gachagua kisa kumzomea kuhusu mikutano ya mradi wa Nyota: “Idler and Jobless”

Oburu pia alitumia fursa hiyo kumkosoa rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kile alichokitaja kama kuitenga ODM katika mipango ya hivi karibuni ya kisiasa ndani ya Azimio.

Alimtuhumu Uhuru kwa kukiuka ahadi za kumfikisha Raila Odinga urais na kuisukuma kando ODM katika ugawaji wa nafasi za Baraza la Mawaziri licha ya handisheki yao.

Mwanasiasa huyo mkongwe alimshutumu kiongozi huyo mstaafu kwa kujaribu kuingilia masuala ya ndani ya ODM, akimtaka ajiondoe.

“Ningependa Uhuru, aliyekuwa Rais. Alikuwa na ndugu yangu baada ya handisheki lakini hakutupa hata kiti kimoja cha baraza la mawaziri na alitudanganya kwamba angemfikisha Raila urais. Alimdanganya Raila kwamba angemfanya rais, ilhali uchaguzi uliibiwa chini ya macho yake na hakufanya chochote. Sasa tunamwomba atuache tufanye tunachotaka kama ODM na aache kuingilia masuala ya ODM,” aliongeza.

Oburu Oginga
Oburu alimuonya Uhuru kujiepusha na masuala ya ODM. Picha: Oburu Oginga.
Source: Facebook

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *