Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakazi waliokuwa wamekimbia mapigano katika mji wa Zawtar al-Gharbiyeh kusini mwa Lebanon wameanza kurejea kufuatia kujiondoa kwa wanajeshi wa Israel, lakini wengi wamekuta nyumba zao zikiwa zimeharibiwa na mali zao zikiwa zimepotea.

Jeshi la Lebanon lilianza kuingia katika mji huo Julai 21, huku wakazi wakianza kurejea Julai 24 baada ya wanajeshi wa Israel kuondoka.

Hatua hiyo ni sehemu ya mpango ulioratibiwa na Marekani na kukubaliwa na Lebanon na Israel kupitia mazungumzo ya moja kwa moja.

Jengo ambalo liliharibiwa katika mashambulio ya Israeli katika Mji wa Zawtar al-Gharbiyeh nchini Lebanon.
Jengo ambalo liliharibiwa katika mashambulio ya Israeli katika Mji wa Zawtar al-Gharbiyeh nchini Lebanon. REUTERS – Zohra Bensemra

Mpango huo unalenga jeshi la Lebanon kuchukua udhibiti wa maeneo husika na kukusanya silaha kutoka kwa kundi la Hezbollah, huku wanajeshi wa Israel wakijiondoa hatua kwa hatua ili kutoa nafasi kwa jeshi la Lebanon kusimamia usalama.

Jeshi la Israel limesema Zawtar al-Gharbiyeh ni mojawapo ya miji mitatu inayotumika kama majaribio ya awali ya utekelezaji wa mpango huo.

Wanajeshi wa Lebanon wakiwa katika Mji wa Zawtar al-Gharbiyeh baada ya wanajeshi wa Israeli kujiondoa.
Wanajeshi wa Lebanon wakiwa katika Mji wa Zawtar al-Gharbiyeh baada ya wanajeshi wa Israeli kujiondoa. REUTERS – Aziz Taher

Hata hivyo, wanajeshi wa Israel bado wanadhibiti ukanda wa takriban kilomita 10 ndani ya kusini mwa Lebanon, ambapo vijiji kadhaa vimeharibiwa kabisa. Maelfu ya wananchi waliokimbia makazi yao tangu vita vya hivi karibuni kati ya Israel na Hezbollah kuanza Machi 2 bado hawawezi kurejea nyumbani.

Wiki iliyopita, milipuko iliyodhibitiwa na jeshi la Israel iliendelea kuripotiwa katika baadhi ya miji iliyo karibu na Zawtar al-Gharbiyeh, jambo linaloonyesha kuwa hali ya usalama katika eneo hilo bado si shwari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *