#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapongeza na kuwashukuru wastaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa kulitumikia Taifa kwa uadilifu na kujituma katika kipindi chote cha utumishi wao.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyoambatana na sherehe za kukaribisha mwaka mpya, Chalamila amekiri kuwa mchango wao umekuwa nguzo muhimu katika ulinzi na usalama wa nchi.
Aidha, RC Chalamila amewatakia wastaafu hao maisha mema na yenye baraka katika hatua hiyo mpya, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kulinda afya zao.
Amewahimiza kutumia uzoefu na weledi mkubwa walioupata jeshini ili kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii na kuwa mfano bora wa uzalendo katika maeneo wanayoenda kuishi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.