Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Donald Trump anapaswa kufahamu kwamba kuingia katika mapambano ya kijeshi na Iran kutakuwa funzo lenye athari kubwa, ambalo matokeo yake yatamzuia kufanya vitisho na majigambo kwenye jukwaa la kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB), Meja Jenerali Mohammad Bagheri Mousavi akijibu matamshi ya hivi karibuni ya Rais Trump wa Marekani, amesema kauli za rais huyo wa Marekani  anayedia kuwa nchi yake ni “nguvu kuu ya dunia”, hazilingani na hadhi ya urais na zinaonyesha wepesi wa fikra na ukosefu wa busara za kisiasa.

Mkuu huyo wa Kamandi ya Majeshi ya Iran ameendelea kwa kuhoji hivi:

“Ikiwa Trump ana nia ya vita, kwa nini wakati huo huo anazungumzia mazungumzo?”

Jenerali Mousavi amesisitiza kuwa, iwapo Marekani itaamua kuanzisha vita dhidi ya Iran, itakuwa inaingia katika vita ambavyo vitakuwa funzo kali, na matokeo yake yatabadilisha namna inavyojiwasilisha kimataifa.

Kauli hizi zinakuja katika muktadha wa mvutano unaoendelea kati ya Tehran na Washington, huku Trump akiendelea kutoa kauli za ubabe na vitisho dhidi ya Iran karibu kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *