Katika kuboresha Maeneo ya kuswalia kwa waumini wa kiisalamu katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara Mbunge wa Viti Maalum Mkoani humo Agness Mathew amekabidhi Busati za kufanyia ibaada katika misikiti yote katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara pamoja na tende huku akiwaomba viongozi msikiti kuendelea kuwa sehemu ya kuwaunganisha watanzania katika umoja.

Agness amekabidhi Busati (ZULIA )hizo ambazo zitasaidia waumini kusali katika Mazingira safi huku akiahidi kutoa ushirikiano wanamna yoyote hiyo.

Awali baadhi ya viongozi wa Miskiti hapa katika Manispaa ya Musoma wamepongeza hatua hiyo kwani bado kuna uhitaji mkubwa wa marekebisho ya Nyumba za ibaada katika Maeneo yao.

“Tunakukuru Sana kwa hiki wengi wamekuwa wqkisahau kukumbuka Nyumba za ibaada lakini ulichokifanya tunakuppngeza Sana Alisema Shekhe Aman kapama Shekhe katika misikiti wa Nyamatare.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Musoma Mkoani Mara Alex Nyabiti Alisema viongozi wa dini wanauwezo mkubwa wakuwaunganisha watanzania nikuhakikisha mshikamano unaendelea kwa wananchi na viongozi wao.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *