Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi amepokea rasmi ombi la Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe la kutaka Nzega ipandishwe hadhi na kuwa mkoa na kuahidi kulifikisha kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya maamuzi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nzega Mjini, mkoani Tabora, Kihongosi amesema hoja ya kuwa mkoa inaungwa mkono na vigezo vya msingi ikiwemo idadi kubwa ya watu, ukubwa wa eneo na uwezo wa halmashauri kujitegemea kiutawala na kifedha.

Aidha amesema ombi hilo linakuja wakati Nzega ikiendelea kunufaika na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Ametaja ujenzi wa mabweni mapya ya kisasa, upanuzi wa shule hadi kidato cha tano na sita, ujenzi wa hospitali ya wilaya yenye vifaa tiba vya kisasa pamoja na maendeleo ya Chuo cha VETA Nzega kuwa ni vielelezo vya ukuaji wa kasi wa eneo hilo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *