
Mashambulizi wa ndege zisizo na rubani (droni) ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF)yameuwa watu watatu na kuwajeruhi wengine saba katika Hospitali ya Al-Mazmoum katika jimbo la Sennar kusini mashariki mwa Sudan.
Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa droni ya wanamgambo wa RSAF iliilenga hospitali ya al Mazmoun na kuuwa watu watatu na kujeruhi saba akiwemo mtoa huduma wa afya.
Tovuti ya Madaktari wa Susdan imelaani shambulio hilo la wanamgambo wa RSF dhidi ya hospitali na kulitaja kuwa limekiuka wazi sheria za kimataifa zinazozuia mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na wafanyakazi wa sekta ya afya.
“Matukio kama haya “yanazidisha mateso ya raia na kuwakosesha huduma za matibabu,” umeeleza Mtandao wa Madaktari wa Sudan.
Wakati huo huo mamlaka husika za Sudan na makundi ya haki za binadamu yamewatuhumu wananamgambo wa RSF kwa kuwashambulia raia. Wanangambo hao hadi sasa hawajatoa taarifa yoyote kujibu tuhuma zinazowakabili.
Shirika la Afya Duniani WHO tarehe 10 mwezi huu lilitahadharisha kuwa mfumo wa afya wa Sudan unakabiliwa na mashambulizi baada ya vito vitatu vya afya katika jimbo la Kordofan Kusini kushambuliwa mwanzoni mwa mwezi huu.
Mapigano makali yameripotiwa katika majimbo matatu ya Kordofan Kaskazini, Magharibi na Kusini tangu mwezi Oktoba 2025 mwaka jana huku mapigano yakiendelea kati ya jeshi la Sudan na RSF.