Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa
Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa
akimshinikiza vikali katika kujaribu kupata suluhu ya vita vya karibu miaka
minne akisema ni jukumu la Kyiv kuhakikisha mazungumzo hayo yanafanikiwa.
Zelenskiy,
katika mahojiano na tovuti ya Marekani ya Axios yaliyochapishwa Jumanne, pia
alisema mpango wowote unaoitaka Ukraine kutoa eneo ambalo Urusi haijaliteka
katika eneo la mashariki mwa Donbas utakataliwa na Waukraine ikiwa utapigiwa
kura ya maoni.
Axios
alimnukuu Zelenskiy akisema “sio haki” Trump kuendelea kutoa
wito hadharani kwa Ukraine, wala si Urusi, kufanya makubaliano katika kujadili
masharti ya mpango wa amani.
“Natumai
ni mbinu zake tu na sio uamuzi,” Axios alimnukuu Zelenskiy alisema katika
mahojiano hayo yaliyofanywa kwa simu wakati wapatanishi wa Urusi, Ukraine na
Marekani walipokuwa wakizungumza mjini Geneva.
Trump
amependekeza mara mbili katika siku za hivi karibuni kwamba ilikuwa ni jukumu
la Ukraine na Zelenskiy kuchukua hatua ili kuhakikisha mazungumzo hayo
yanafanikiwa.
“Ni
vyema kwa Ukraine ije katika meza ya mazungumzo haraka. Hayo ndiyo ninayokuambia,”
Trump aliwaambia waandishi wa habari ndani ya Air Force One siku ya Jumatatu.
Soma zaidi: