Waziri wa Jihadi ya Kilimo wa Iran ametangaza ongezeko kubwa la mauzo ya nje ya kilimo hapa nchini hadi dola bilioni nane na kutangaza kwamba asilimia 85 ya usalama wa chakula wa Iran inadhaminiwa na uzalishaji wa ndani.

Gholamreza Nouri Ghezeljeh, Waziri wa Jihad ya Kilimo wa Iran, amesema hayo katika mkutano wa kukagua uagizaji wa bidhaa za msingi na pembejeo za mifugo na kubainisha kwamba, “Uuzaji wa bidhaa za kilimo nje ya Iran umeongezeka kwa dola bilioni tatu, kutoka dola bilioni tano mwaka jana hadi dola bilioni nane.” Akizungumzia uagizaji wa bidhaa za msingi, alisema: “Kwa sasa, dola bilioni 16 za bidhaa za msingi na za kilimo zimeingia nchini, jambo ambalo linakidhi baadhi ya mahitaji muhimu.”

Akisisitiza utegemezi mdogo wa Iran kwa uagizaji wa bidhaa za kilimo, Waziri wa Jihadi ya Kilimo wa Iran amesema: “Kwa upande wa uzito, asilimia 85 ya usalama wa chakula inadhaminiwa na uzalishaji wa ndani na asilimia 15 kwa uagizaji.” Kwa upande wa thamani ya tani, Nouri Ghezeljeh pia alisema kwamba sehemu ya uzalishaji wa ndani ni asilimia 80 na uagizaji ni asilimia 20. Takwimu hizi zinaonyesha utoshelevu mkubwa wa Iran katika kukidhi mahitaji ya chakula ya watu.

Iraq, ikiwa na ununuzi wa dola bilioni 1.4, ikifuatiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu dola milioni 531 na Russia dola milioni 376, ni nchi zinazoongoza kwa mauzo ya nje ya Iran. Pakistani, Afghanistan, China na India pia ziko katika safu inayofuata. Takwimu hizi zinaonyesha utofauti wa masoko lengwa na ongezeko la ubora wa bidhaa za kilimo za Iran ili kushindana katika uwanja wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *