Jeshi la Congo, FARDC linawashutumu wanajeshi wa Rwanda wanaoshirikiana na waasi wa AFC/M23 kushambulia maeneo yake kwenye jimbo la Kivu Kaskazini na Kusini, likisema vitendo hivyo vinakiuka mpango wa usitishaji mapigano uliopendekezwa na rais wa Angola, João Lourenço.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa yake iliyotolewa Ijumaa hii, FARDC imesema tarehe 18 na 19, wanajeshi wanaodhaniwa kuwa wa Rwanda wakishirikiana na waasi wa M23, walishambulia kambi zake huko Ihula, Kazaraho, Bugabo, Cahi na Virumbi jimboni Kivu Kaskazini.

Aidha FARDC inasema katika jimbo la Kivu kusini, vijiji vya Mikenge na Kalonge huko Fizi na Uvira vilishambuliwa pamoja na miji ya Kahungwe, kanga na Lugeje.

Maelfu ya raia wa mashariki ya DRC wametoroka mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali FARDC.
Maelfu ya raia wa mashariki ya DRC wametoroka mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali FARDC. AFP – JOSPIN MWISHA

Taarifa ya jeshi la Congo, imeongeza kuwa vitendo vinavyofanywa na Rwanda pamoja na waasi wa M23 ambavyo ni vyamakusudi, vinakusudia kutatiza mchakato wa amani unaoendelea, FARDC kwa upande wake ikidai itaendelea kuheshimu makubaliano yaliyopo.

Kwa upande wake waasi wa M23 katika taarifa waliyoitoa Februari 19, walilituhumu jeshi la Serikali na washirika wao kushambulia maeneo wanayoyakalia katika milima ya jimbo la Kivu Kusini, na kwamba linakiuka makubaliano ya Doha na Qatar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *