Mtandao wa kigaidi wa JNIM wenye uhusiano na Al Qaeda, umeendelea kupanuka nje ya mipaka ya Sahel hadi katika pwani ya Afrika Magharibi, ingawa unasita kuanzisha makazi ya kudumu, ripoti mpya ya shirika la kimataifa la utatuzi wa mizozo imeonesha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kundi hili ambalo lilianzishwa mwaka 2017, limejipambanua kama moja ya kundi muhimu la kijihadi kwenye êneo la Sahel, ambako linadhibiti maeneo kadhaa ya Burkina Faso, Mali na Niger.
Kwa mujibu wa ICG, tangu mwaka 2019 kundi hilo lilipanua wigo wa opresheni zake katika pwani ya Ghuba ya Guinea, ambako lilisimika vituo vyake vya usafirishaji na kutekeleza mashambulizi mfululizo kuongeza udhibiti.
Hata hivyo ripoti ya ICG imesema kujitanua kwa kundi hili kunaweza kuwa na athari kwa mkakati wake wa kuendelea kuwa na udhibiti wa maeneo zaidi ya Afrika Magharibi.
Aidha ripoti imeonya kuwa kupanuka kwa mtandao wa kundi hilo kunahatarisha usalama wa mataifa zaidi ya Afrika Magharibi, ikiwemo Benin na Togo.