Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi ametembelea msibani kwa Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo kuwasilisha salamu za rambirambi.

Dk Nchimbi ametembelea msibani hapo, kuwasilisha salamu za rambirambi za Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni siku moja tangu kufariki dunia kwa Kardinali Pengo, aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Kardinali Pengo alifariki dunia saa 4:00 usiku wa Februari 19, 2026, akiwa na umri wa miaka 82, huku akitumia miaka zaidi ya 40 kulitumikia kanisa kwa nafasi mbalimbali ukiwemo upadri, uaskofu hadi kardinali.

Taarifa ya Dk Nchimbi kutembelea msibani hapo yalipo makazi ya kiaskofu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Kurasini imetolewa leo, Ijumaa Februari 20, 2026.

Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi ametembelea msibani kwa Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo kuwasilisha salamu za rambirambi.

Katika mazungumzo yake na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Thaddeus Ruwa’ich, Dk Nchimbi amesema Rais Samia ameguswa na msiba huo.

Amesema mkuu huyo wa nchi ameahidi kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Kanisa Katoliki katika kipindi cha maombolezo.

Ameeleza Serikali inatambua mchango alioutoa Kardinali Pengo katika miaka 42 ya utumishi wake wa kiroho na kijamii na kusisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha anazikwa kwa heshima zote zinazostahili.

Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi ametembelea msibani kwa Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo kuwasilisha salamu za rambirambi.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu Ruwa’ichi ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na mchango wake, hususan katika kipindi cha matibabu ya Kardinali Pengo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *