Wananchi wa Wilaya ya Nyang’hwale sasa wanaweza kupata huduma za afya kwa faragha zaidi baada ya Hospitali ya Wilaya ya Nyangh’wale kuanzisha wodi maalum kwa wagonjwa wanaohitaji utulivu na huduma binafsi.
Mkurugenzi wa Halmashauri hya Wilaya ya Nyangh’wale Husna Toni amesema wodi hizo za faragha zinatoa huduma bora chini ya wataalamu wa afya waliopo hospitalini hapo kwa gharama nafuu ambapo Wagonjwa wasio na bima ya afya huchangia shilingi elfu 15 kwa siku, huku wenye bima wakigharamia shilingi elfu 10 tu.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya maboresho yanayoendelea katika hospitali hiyo, yenye lengo la kusogeza huduma bora karibu na wananchi na kupunguza ulazima wa kusafiri nje ya wilaya kutafuta matibabu
#startvupdate
(Feed generated with FetchRSS)