Tanzania na Zambia zimefanikiwa kutatua kero tano kati ya kumi zilizokuwa zikiwakabili madereva wa malori katika mpaka wa Tunduma na kusababisha foleni kubwa ya maroli, huku zilizobaki zikiendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Hatua hiyo imefikiwa katika kikao cha pamoja kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia, Mulambo Haimbe ambapo miongoni mwa maamuzi muhimu ni kuanza kwa utoaji huduma wa saa 24 kwa pande zote mbili za mpaka, hatua iliyotajwa kuwa suluhisho muhimu kwa changamoto ya muda mrefu ya madereva.
#AzamTVUpdates
✍Joyce Lyanda
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)