Muendesha baiskeli rai awa Uhispania Pau Soriano, hapo jana alifanikiwa kushinda hatua ya pili ya mashindano ya Tour du Rwanda, akimshinda kwa mbali Mueritrea Henok Mulubrhan.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Pau mwenye umri wa miaka 21, anaendesha baiskeli ya kampuni ya NSN Development, alimaliza umbali wa kilometa 134.6 kutoka Nyamata hadi Huye akitumia mud awa saa 3, dakika 10 na sekunde 10.30.

Aidha mwendesha baiskeli wa kampuni ya Lotto, Mauro Cuylits, yeye alimaliza katika nafasi ya tatu.

Matokeo ya hatua ya pili kwa ujumla yalikuwa:

  1. Marti Soriano Pau (NSN Development Team) – 3h 10’10”
  2. Henok Mulubrhan (Eritrea) – +0.02”
  3. Mauro Cuylits (Lotto–Groupe Wanty) – +0.13”
  4. Muñoz Gabina Hodei (Soudal Quick-Step Devo Team) – +0.43”
  5. Van Gils Lucas (Lotto–Groupe Wanty) – +0.54”

Leo ni hatua ya 3: Kutoka Huye kwenda Rusizi umbali wa kilometa 145.3.

Katika hatua nyingine shirikisho la mchezo wa baiskeli nchini Rwanda, FERWACY, limeahidi kuongeza udhibiti wa masuala ya usalama kwenye mashindano ya mwalka huu, kufuatia ajali iliyohusisha msafara wa magari ya matangazo ambapo watu wawili waligongwa na kufariki dunia kwenye wilaya ya Gatsubo wakati wa hatua ya kwanza.

Kufuatia tukio hilo polisi walianzisha ushunguzi, ambapo pia tangu jana walikuwa wakiwapima madereva wa magari kiwango cha ulevi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *