Mdau wa michezo, shabiki na mwanachama wa Young Africans Sports Club (Yanga) kutoka Geita, Hussein Makubi maarufu Mwananyanzala, ameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kwa timu itakayoshinda dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba Sports Club.
Dabi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuchezwa Machi Mosi, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geita, Mwananyanzala amesema dau hilo ni sehemu ya kuhamasisha ushindani na kuongeza morali kwa wachezaji wa timu zote mbili.

Mwananyanzala amewataka mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo linalochukuliwa kama nembo ya soka la Tanzania, akisisitiza mashabiki wa Yanga kusafiri kwa wingi kwenda Zanzibar kuiunga mkono timu yao.
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *