- Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua ameendelea kuhamasisha uungwaji mkono kwa upinzani wa pamoja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027
- Gachagua alimkosoa Raila Odinga kuhusu urithi wake wa kisiasa, akidai aliitelekeza jamii ya Abagusii alipokuwa serikalini
- Kauli za Gachagua zilizua hisia mseto miongoni mwa Wakenya kuhusu miungano ya kisiasa na uongozi
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ameendelea kuhamasisha uungwaji mkono kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i kuelekea uchaguzi wa 2027.

Source: Facebook
Matiang’i ndiye mgombea urais wa Jubilee Party, huku Gachagua akiongoza Democracy for Citizens Party (DCP), vyote vikiwa chini ya muungano wa upinzani wa pamoja.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika kaunti ya Kisii Jumanne, Februari 24, Gachagua aliwahimiza wakazi kumchagua kiongozi atakayewawakilisha moja kwa moja kwenye meza ya kitaifa.
Je, Raila aliitelekeza jamii ya Kisii baada ya kujiunga na serikali?
Gachagua aliikumbusha jamii hiyo kuhusu uungwaji mkono wao wa muda mrefu kwa kiongozi wa ODM, hayati Raila Odinga, ambaye alidaiwa kuwatelekeza baada ya kujiunga na serikali zilizopita.

Pia soma
Magazeti ya Kenya: NIS yamhusisha mwanachama wa UDA na sakata ya Wakenya kuingia jeshi la Urusi
Alikosoa miungano ya Raila ya zamani, akidai ilikuwa kwa manufaa binafsi licha ya uungwaji mkono mkubwa wa jamii.
“Jamii ya Abagusii imepitia changamoto nyingi. Mlikuwa mkitumia dalali kutoka ODM kufika kwenye meza ya kitaifa. Kila alipoingia serikalini, alikula peke yake na kuwaacha mkihangaika. Safari hii mmepata kiongozi atakayewawakilisha moja kwa moja mahitaji yenu serikalini. Je, Matiang’i anafaa kuwaongoza? Tunawaomba kama viongozi mtupatie Matiang’i ili twende tukaunde serikali,” alisema Gachagua.
Ingawa Raila alipoteza katika chaguzi tano, aliwahi kushiriki katika serikali za marais wa zamani Daniel Moi, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta.
Kabla ya kifo chake cha ghafla Oktoba 2025, Raila na Rais William Ruto waliunda mpango wa ushirikiano mpana uliounganisha vyama vya UDA na ODM, na kusababisha uteuzi wa wataalamu wanne wa ODM katika Baraza la Mawaziri la Ruto.
Licha ya mpango wa kuvunjwa kwa muungano huo kufikia 2027, baadhi ya viongozi wa ODM kuunga mkono kuchaguliwa tena kwa Ruto kumezua mgawanyiko ndani ya chama. Miongoni mwa wanaounga mkono mpango huo ni gavana wa Kisii Simba Arati.
Kauli za Gachagua zilimghadhabisha aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Town Ngunjiri Wambugu, ambaye alimshutumu kwa kuendelea kumkashifu Raila hata baada ya kifo chake.
“Yaani Jofri hana adabu kabisa. Alimtukana Baba akiwa hai na anaendelea kumtukana hata baada ya kifo!” alisema.
Wakenya walijibu vipi kauli za Gachagua?
Dionte Okemwa: “Ukweli haujali kama uko hai au la… fanya tu jambo sahihi ukiwa hai.”
Njoro Deepsea: “Siku hizi hakuna kupitia dalali, madalali wataisha wote.”
Benard Onyango: “Kwa hivyo Wakisii ndio wanafaa kupiga kura ndio Matiang’i awe rais? Wacha tuweke macho, huyu mkabila ameanza kuharibu maneno sasa.”
Daniel Kadenge Khwa Barasa: “Heshima hupatikana, si kudaiwa. Uongozi ni unyenyekevu na adabu, si vitisho. Mtu akidhani anaweza kunyamazisha viongozi kwa vitisho, amekosea. Wananchi, si watu binafsi, ndio huamua nani aende nyumbani kutoka bungeni.”
Catherine Wambui: “Jofri ni mgonjwa.”
Eunice Nice: “Wenye wanafuata huyu jamaa wana kasoro.”
Evans Kasmai Kiptulon: “Yeye sasa ni dalali… anataka kuwa dalali wa Wakikuyu kwa Matiang’i ama kwa Kalonzo kupitia DCP… Hata amesahau anaanza kujisema.”

Source: Facebook
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
