.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Kunyoa nywele kwa wanawake na wanaume, ni jambo ambalo ni lazima kwa wengi ili kudumisha usafi, afya na urembo.

Wengine hunyoa nywele kila wiki,kila mwezi, wengine si kila mara, ila kila mtu ana muda wake wa kunyoa nywele.

Ila wakati mwingine, njia sahihi huwa hazifuatwi katika harakati hii.

Iwapo usafi na afya hautazingatiwa wataalam wanaonya magonjwa mengi yatasambaa.

Wakati mwingi watu huwa na wasiwasi kuhusu mtindo na urembo wataopata baada ya kunyoa, bila ya kujali vifaa vitakavyotumika.

Ingawa sasa kuna vifaa vya kisasa vya kunyoa nywele, bado kuna hatari ya magonjwa kusambaa kwa viwango sawa kama awali ambapo watu walikuwa wakitumia wembe, makasi na visu vidogo.

Hatari ya kuambukizwa magonjwa katika duka la mitindo ya nywele/salon iko juu iwapo usafi wa vifaa hautazingatiwa.

Wakati mwingine ajali hutokea wakati mtu ananyolewa kama kujikata kwenye kichwa na majeraha madogo ambayo mtu hawezi kuyaona kwa urahisi.

Aidha wataalam wa afya wanasema kuwa majeraha hayo madogo ndio huwa vyanzo vya kuambukizana magonjwa, iwapo vifaa vinavyotumika si visafi.

Cha kuhofu ni kuwa, dalili za magonjwa huwa hayaonekai kwa haraka, wengine huanza kuwashwa, kupata uvimbe au kuanza kupoteza nywele bila kujua tatizo liko wapi, anasema Dkt. Sani Abubakar mtaalam wa afya ya umma.

Dkt. Sani anasema magonjwa mengi ya ngozi haswa kichwani hutokana na uchafu katika sehemu za kusuka na kunyoa nywele.

Kulingana naye ‘kifaa chochote kinachokuja karibu na ngozi yako, iwapo mtu aliyetumia awali alikuwa amejeruhiwa, inaweza kuwa chanzo cha kuambukizwa magonjwa.’

Daktari huyo anataja magonjwa ambayo mtu anaweza kupata katika vinyozi na maeneo ya kusuka nywele.

Ugonjwa wa fangasi(Ringworm)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Dkt. Sani anasema ugonjwa huu hupatikana kama wembe au kichana unachotumia kilitumiwa na mtu aliye na maradhi ya ngozi kama eczema or psoriasis.

“Ugonjwa huu hufanya ngozi ya kichwa kuwa na ungaunga au magamba, na baadaye kusababisha mtu kuanza kupoteza nywele.”

Hepatitis B (Homa ya Manjano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hepatitis C

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ugonjwa huu pia husambzwa kwa njia ya damu. Dkt. Sani anaelezea kuwa kutobadilisha wembe au kutosafisha vifaa vya kunyoa husambaza viini vya maradhi haya.

HIV/AIDS

Ingawa si rahisi,Dkt. Sani anasema kuna uwezekano wa kupata virusi vya Ukimwi iwapo mtu aliyeambukizwa atakatwa na wembe wa kunyoa na kisha kifaa hicho kutumiwa na mtu mwingine.

Uvimbe katika ngozi ya kichwa

Dkt. Sani anaelezea kuwa ugonjwa huu hutokea wakati bakteria inaingia kwenye Ngozi baada ya kunyoa, na kusababisha uvimbe haswa kwenye kisogo.

Upele

Ingawa ugonjwa huu hauhusiani moja kwa moja na kunyoa nywele, daktari anasema huenda ikaletwa na matumizi ya taulo chafu au vifaa vichafu vya kunyolea.

Jinsi ya kujilinda

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Dkt Sani anaelezea kuwa hakikisha unatumia wembe mpya wakati wa kunyoa, vifaa vya kunyoa vinasafishwa kabla ya kutumika, usinyoe sehemu ambayo ina kidonda, wazazi wanafaa kuwa waangalifu na watoto wao wanaponyoa, na ni vyema kumiliki vifaa vyako vya kunyoa.

Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *