#HABARI: Wananchi wa Kata ya Shiwinga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, wameshiriki zoezi la upigaji kura kumchagua diwani mpya atakayeziba nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Lusekelo Mwalukomu aliyefariki dunia mwaka 2025.

Jumla ya vyama nane vya siasa vimechuana katika uchaguzi huo, huku wapiga kura 6,854 wakitarajiwa kutekeleza haki yao ya kikatiba katika vituo mbalimbali vilivyopangwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Wakizungumza wakati wa zoezi hilo, wananchi wamepongeza hali ya utulivu na maandalizi mazuri ya Tume, wakibainisha kuwa mchakato huo umegubikwa na amani tangu asubuhi.

Wakazi hao wameeleza matarajio yao kuwa kiongozi atakayeibuka mshindi atakuwa chachu ya maendeleo kwa kutatua kero za kijamii na kiuchumi zinazoisumbua kata hiyo, hususan katika kuboresha miundombinu na huduma za afya.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *