#HABARI: Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC) imeeleza kuvutiwa na mikakati ya Tanzania katika kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, hususan hatua ya kuondoa kodi na kutoa ruzuku kwa vifaa kama mitungi ya gesi na majiko banifu, pamoja na kampeni za uhamasishaji kwa wananchi.
Akizungumza katika mdahalo wa Mawaziri kuhusu Nishati endelevu katika maadhimisho ya Wiki ya Nishati Endelevu ya SADC inayofanyika Victoria Falls, Zimbabwe (23–27 Februari 2026), Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba amesema Tanzania inalenga kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, huku Mpango Mahsusi wa Taifa wa Nishati ukilenga asilimia 75 ifikapo 2030.
Mhe. Salome amesema Serikali imeweka mkazo kwa taasisi zinazohudumia zaidi ya watu 100 zikiwemo magereza, kambi za jeshi, shule na masoko makubwa kwa kuzifungia mifumo ya nishati safi ya kupikia, hatua iliyotajwa kuwa ya ubunifu na yenye matokeo chanya.
Aliongeza kuwa Tanzania imefikisha umeme katika vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara, na kuongeza upatikanaji wa umeme hadi asilimia 85.5. Uwezo wa uzalishaji umefikia megawati 4,437 na unatarajiwa kuongezeka hadi megawati 8,000 ifikapo 2030.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Magosi aliipongeza Tanzania kwa kuongoza juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika Ukanda, hivyo kuchochea mabadiliko chanya ya kijamii, kiuchumi na kimazingira katika ngazi zote za maendeleo.
Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Constantino Chiwenge amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kutumia rasilimali za nishati jadidifu kama chachu ya maendeleo ya kiuchumi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.