#HABARI: Mbunge waJimbo la Kawe jijini Dar es Salaam Mhe. Geofrey Timoth, amewahakikishia wafanyabiashara wadogo (wauza maua), waliokuwa wakifanya shughuli zao katika eneo la Kawe lililopo chini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuwa wataendelea na biashara zao baada ya kupatiwa eneo mbadala wakati utekelezaji wa mradi wa maendeleo ukiendelea.
Timoth amesema awali wafanyabiashara hao walipewa taarifa ya kuondoka kupisha mradi wa maendeleo, lakini aliingilia kati na kufanya mazungumzo na uongozi wa NHC ili kuhakikisha wanapata suluhisho litakalolinda maslahi yao.
Ameeleza kuwa NHC imekubali kutowondoa wafanyabiashara hao kabisa, bali imeandaa utaratibu wa kuwahamishia katika eneo la karibu, ili waweze kuendelea na shughuli zao bila kuvuruga utekelezaji wa mradi huo.
Mbunge huyo amewahakikishia wafanyabiashara hao wa maua kuwa wataendelea kufanya biashara zao kwa amani na utulivu chini ya utaratibu utakaoainishwa na NHC.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania