#HABARI: Wagombea Ubunge wa Jimbo la Peramiho kutoka Vyama Vya Siasa 14 NLD, AAFP, MAKINI, UMD, UPDP, DP, CCK, TLP, UDP, SAU, NCCR MAGEUZI, ADA TADEA na ADC vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa sura ya 258, kwa umoja wao wameamua kuja na tamko la pamoja kuhusiana na mwenendo wa mchakato mzima wa Uchaguzi mdogo wa marudio wa Jimbo la Peramiho uliofanyika Februari 26.

Kwenye tamko lao wamesema “kwanza, tunaipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kwa kuhakikisha mchakato mzima wa Uchaguzi uliofanyika kwa haki na amani tangu wakati wa uchukuaji fomu za kugombea Ubunge, ambapo nyinyi wenyewe (INEC) mmeona safari hii hujasikia Chama chochote kikilalamika kuhusu mgombea wake kukatwa au kukatishwa ndoto yake ya kugombea ndani ya Jimbo la Peramiho”

Wamesema INEC imehakikisha wanatenda haki wakati wa upangaji ratiba wa mikutano ya kampeni, na hakuna Chama ambacho kiliingilia ratiba ya Chama kingine cha siasa na hata ilipotokea changamoto za kawaida, INEC ilibaki kama walezi wawagombea wote na ikatenda haki kwa usawa.

Pia tamko wamempongeza Dkt. Lazaro Kiliani Komba Bunungu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi alioupata.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *