Serikali imesema kiwango cha ajira za watoto nchini kimeendelea kupungua kutoka asilimia 33 mwaka 2014 hadi asilimia 25.8 mwaka 2024 kutokana na juhudi za pamoja za serikali na wadau wa maendeleo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira za Watoto, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesema serikali imejipanga kutokomeza kabisa tatizo hilo ifikapo mwaka 2030.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *