Wakati mwili wa mwanafunzi Rebeca John Miswungwi wa Chuo cha St John University kilichopo jijin Dodoma ukiagwa jana maswali wanafunzi wenzake pamoja na ndugu wa mwanafunzi huyo wameibua maswali kuhusiana na kifo hicho wakidai si cha kawaida.

Mwili huo unasafirishwa kuelekea nyumbani Kwa wazazi wake Jijini Mwanza kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Mwanafunzi huyo anadaiwa kufariki dunia baada ya kuungua na moto ambao bado haujajulikana chanzo chake.

Hata hivyo, ndugu wa marehemu wamedai kuwa chanzo cha tukio ni ugomvi ulioambatana na wivu wa kimapenzi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *