
Mahakama ya rufaa nchini Tunisia, imepunguza kifungo cha aliyekuwa Wazriri Mkuu Ali Larayedh kutoka miaka 34 hadi 24 jela, baada ya kupatikana na kosa la ugaidi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hukumu hii imekuja baada ya Waziri Mkuu huyo wa zamani kukamatwa mwishoni mwa mwaka 2022, akidaiwa kuwatuma wanajihadi kwenda kupigana nchini Iraq na Syria.
Hata hivyo, hadi kuhukumiwa kwake jela, Larayedh, amekanusha tuhma hizo akisema, zimechochewa kisiasa kwa sababu ni mpinzani na mkosoaji mkubwa wa rais Kais Saied.
Kifungo hiki kipya kimekuja baada yam waka uliopita, kuhukumiwa jela miaka 34, kwa kosa hilo ambalo Mawakili wake walikata rufaa.
Larayedh mwenye umri wa miaka 70, alikuwa Waziri Mkuu wa Tunisia kati ya mwaka 2013 hadi 2014, wakati huo akiongoza chama cha Kiislamu cha Ennahdha, kilichoongoza nchi hiyo kwa kupindi kifupi baada ya mapinduzi ya wananchi mwaka 2011.