Kazi ya kutoa huduma ya malezi kwa wagonjwa haswa nyumbani mara nyingi hutafsiriwa kuwa upendo, lakini nyuma ya pazia walezi wa muda mrefu hubeba mzigo mzito, na hata kukabiliwa na changamoto za afya ya kihisia na kiakili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwanahabari wetu Jupiter Mayaka ametembelea mlezi mmoja kaunti ya Kiambu nchini Kenya, aliyejinasua kutoka kwenye sonona ( Depression) kupitia  kutunza maua.

Ninapoingia katika makaazi ya Irene Kui, macho yangu yanavutiwa na bustani zuri lenye maua ya aina tofauti.

Kwa miaka kadhaa, Kui alipambana na msongo wa mawazo. Karibu umsababishie sonona alipokuwa anamtunza mumewe aliyepoteza uwezo wa kutembea kutokana na tatizo la kiafya, lakini aligundua uponyaji katika bustani lake.

‘‘Haya mambo yenye nilikuwa napitia ya stress, karibu niingie kwenye sonona watu wengi sana wanapsitia, lakini wataambia nani? Umewahi ona mama anajiongelesha tafadhali usimhukumu ako therapy. Kitu kingine, ukikuja hapa kwa maua uongeleshe maua, haitawahi kukusengenya.’’

Kui anasema kuna haja ya kutoa mafunzo kwa walezi. 

‘‘Wangapi wanauliza mawazo yako yakoje leo, ulilalaje, uliamkaje, hata wasiwapatie hii elfu mbili, hakikisha tu hospitali kuna dawa, kuna mashine, SHA inafanya, shida za walezi zitakuwa zimepungua kwa asilimia 70.’’

Aidha anaeleza changamoto kuu inayowakabili walezi wengi wnaowahudumia wagonjwa wao majumbani.  

‘‘Ninatamani kungekuwa vile ukitoka hospitali daktari anakuambia huu mpatie chakula hiki, kama kungekuwa vile sisi sote tungejifunza uuguzi, au walezi wapewe maarifa ya kimsingi.’’

Mwanasaikolojia Beverly Achieng anasema mazingira yana mchango mkubwa katika kupunguza msongo wa mawazo na sonona.

‘‘Mazingira yanaathiri sana afya ya akili watu wakiwa karibu na mimea, hizo homoni za msongo wa muda mrefu inapunguzwa. Mwili unaingia katika hali ya utulivu hali ya kupumzika na kujirekebisha.‘’

Shirika la Caregiver Action network, linasema uchunguzi unaonesha kuwan walezi wanaotunza wapendwa wao hukabiliwa na mfadhaiko kwa viwango vya juu mara sita kuliko wasio walezi

Jupiter Mayaka, Nairobi RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *