
“Kutokana na hali ya usalama, wafanyakazi wa Uingereza wameondolewa kwa muda kutoka Iran. Ubalozi wetu unaendelea kufanya kazi kwa njia ya video,” Wizara ya Mambo ya Nje imesema kwenye tovuti yake. Wizara ya Mambo ya Nje tayari ilikuwa imetangaza kufungwa kwa muda kwa ubalozi wake huko Tehran katikati ya mwezi Januari.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
China pia imewataka raia wake leo Ijumaa kuondoka nchini Iran “haraka iwezekanavyo,” wakati Tehran ikikabiliwa na vitisho vya mara kwa mara vya mashambulizi ya anga ya Marekani.
“Kwa kuzingatia hali ya usalama iliyopo sasa nchini Iran, Wizara ya Mambo ya Nje ya China na balozi na balozi ndogo za China nchini Iran zinawakumbusha raia wao kuepuka kusafiri kote nchini wakati huu,” Idara ya Masuala ya Kibalozi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Beijing imeeleza katika taarifa.
Wizara hiyo imehakikisha kwamba balozi na balozi ndogo za China nchini Iran na nchi jirani zitatoa “msaada unaohitajika” kwa raia wa China wanaotaka kuondoka nchini humo kwa ndege za kibiashara au nchi kavu.
China pia iliwaomba raia wake nchini Israel kuendelea kuwa macho na kuimarisha tahadhari zao za usalama.
Marekani, kwa upande wake, imependekeza leo Ijumaa kwamba wafanyakazi wasio wa lazima katika ubalozi wake mjini Jerusalemu waondoke Israel, huku kukiwa na vitisho vya Marekani vya mashambulizi dhidi ya Iran, na kuzua hofu ya mapigano ya kikanda.
Matangazo haya yanakuja siku moja baada ya duru ya tatu ya mazungumzo huko Geneva, yaliyosimamiwa na Oman, kati ya Tehran na Washington, yanayoonekana kama jaribio la mwisho la kuepuka vita, baada ya Marekani kutumwa meli za kivita na wanajeshi wengi Mashariki ya Kati katika miongo kadhaa.