Rais wa Marekani ametangaza kwamba nchi yake imetekeleza shambulio kubwa dhidi ya Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Rais Trump, nchi yake itaharibu jeshi la majini la Iran pamoja na kusambaratisha kabisa vituo vyake vya kujenga makombora.

Aidha Rais Trump ametoa wito kwa raia wa Iran kuutumia wakati huu wa mashambulio kuchukua serikali yao.

Katika ujumbe wake wa video baada ya Marekani na Israel kuanza kuishambulia Iran, Trump amesisitiza kuwa lengo la mashambulio hayo ni kuangusha utawala wa Iran.

Trump aidha ametoa wito kwa wanajeshi wa Iran na walinda usalama maalum waliopewa jukumu la kuilinda serikali ya Iran kujisalimisha.

Mwezi Juni mwaka uliopita, Rais Trump aliagiza jeshi la Marekani kushambulia kwa mabomu vituo vya silaha za nyukilia vya Iran, mashambulio yaliofanyika kwa ushirikiano na Israel.

Trump amekuwa akisisitiza kwamba anataka mabadiliko ya uongozi nchini Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *