Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deo mwanyika, amewaasa watanzania wenye uwezo kujitoa katika kuwasaidia wasio na uwezo katika kipindi hiki ambacho wakristo na Waislamu wako katika funga ya Kwaresma Ramadhan.

Mwanyika ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Njombe mjini ametoa wito huo wakati akikabidhi mahitaji mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Mil.2 katika msikiti wa wilaya ya Njombe kwaajili ya futari.

Kupitia waratibu wa ofisi yake Chrispin Kalinga amesema katika kipindi hiki cha funga ya kwaresma na Ramadhan wapo watu wanaotamani kufuturu lakini hawawezi kufanya hivo kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, hta hivyo ni wakati sahihi wa wale wanaojiweza kujitoa kuwashika mkono ili waweze kujisikia furaha kama wengine.

#RFAOnline
#HabariStartv
@dkhan1410.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *