
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema nchi yake inakabiliwa na awamu yenye changamoto zaidi katika historia yake ya hivi karibuni huku kukiwa na msukosuko wa kimataifa.
Merz ameyasema hayo leo wakati akitetea bajeti inayopendekezwa na serikali yake kwa mwaka wa fedha wa 2026 katika mjadala mkuu wa bunge la Ujerumani, Bundestag.
Kiongozi huyo ameamua kusalia mjini Berlin kushughulikia masuala ya ndani ya nchi na kutohudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York, Marekani.
Hali ya wasiwasi ya kimataifa ilikuwa mada kuu ya hotuba yake kwa wabunge huku akiweka wazi kwamba nchi za Magharibi kwa sasa zinakabiliwa na hali mbaya kufuatia mizozo ya kivita na ya kibiashara inayoendelea duniani.