Kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2026, fahamu timu ya mfano ya wakimbiziKuelekea fainali za Kombe la Dunia 2026, fahamu timu ya mfano ya wakimbizi

Bernard Kamungo,  raia wa Marekani ambaye alikulia kwenye kambi ya wakimbizi huko Kasulu, mkoani Kigoma nchini Tanzania; Awer Mabil, aliyezaliwa katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya na Nestory Irankunda aliyezaliwa katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania ni miongoni mwa wachezaji 11 waliotangazwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.

Wanaunda timu maalumu ya mfano ambapo wengi wao watashiriki matukio mbali mbali wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Mexico, Marekani na Canada.

Katika taarifa kutoka mjini Geneva, UNHCR imesema timu hiyo inayojulikana kama “Kikosi cha kuleta Mageuzi” inalenga kuhamasisha mashabiki wa soka pamoja na wakimbizi duniani kuamini kuwa inawezekana kushinda changamoto za maisha kupitia usalama, fursa na msaada wa jamii.

Mchezaji wa mpira wa miguu Antonio Rüdiger, amevaa T-shirt ya UNHCR, akitabasamu akiwa na mikono iliyounganishwa kwenye uwanja.

© UNHCR/Rafael Greilberger Antonio Rüdiger, Mchezaji mlinzi wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani, hutumia jukwaa lake kusaidia wakimbizi na kutetea jamii zilizohamishwa.

Wachezaji, asili yao na timu zao

  • Nahodha ni Alphonso Davies anayechezea imu ya taifa ya Canada na balozi mwema wa UNHCR. Yeye alizaliwa  katika kambi ya wakimbizi nchini Ghana baada ya wazazi wake kukimbia vita nchini Liberia
  • Bernard Kamungo: Mchezaji wa FC Dallas ya Texas nchini Marekani, aliyekulia katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania kabla ya kuhamishiwa Marekani. Ameiwakilisha timu ya taifa ya Marekani.
  • Awer Mabil: Mchezaji wa CD Castellón, aliyezaliwa katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya na kuichezea Australia katika Kombe la Dunia.
  • Nestory Irankunda: Mchezaji wa Watford FC, aliyezaliwa na wazazi warundi katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania na kuhamishiwa Australia, ambako anaiwakilisha timu ya taifa.
  • Antonio Rüdiger ambaye wazazi wake walikimbia vita nchini Sierra Leone na kupata hifadhi nchini Ujerumani.
  • Asmir Begović: Mchezaji wa Leicester City FC ya Uingereza, aliyekimbia Bosnia akiwa na umri wa miaka minne, na kuiwakilisha Bosnia na Herzegovina katika Kombe lao la Dunia la kwanza.
  • Ali Al-Hamadi: Mchezaji wa Luton Town FC ya Uingereza, aliyekimbia Iraq kutafuta usalama nchini Uingereza, na kusaidia Iraq kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40.
  • Eduardo Camavinga: Mchezaji wa Real Madrid ya Hispania ambaye wazazi wake waliishi kipindi cha vita nchini Angola na kuanza maisha mapya nchini Ufaransa. Sasa anachezea timu ya taifa ya Ufaransa.
  • Victor Moses: Mchezaji wa FC Kaisar, aliyekimbia Nigeria kutafuta usalama nchini Uingereza na baadaye kuiwakilisha Nigeria.
  • Mohamed Touré: Mchezaji wa Norwich City FC ya Uingereza, aliyezaliwa akiwa mkimbizi nchini Guinea na kuhamishiwa Australia, na sasa anaiwakilisha timu ya taifa ya Australia.
  • Ermedin Demirović: Mchezaji wa VfB Stuttgart. Baba yake alikimbia Bosnia na kujenga maisha mapya nchini Ujerumani, ambako Ermedin alizaliwa na kulelewa. Anaichezea timu ya taifa ya Bosnia na Herzegovina na kusaidia timu hiyo kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya pili.

Soma taarifa nzima hapa na kauli za viongozi na wachezaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *