Wimbi la 15 la Operesheni Ahadi ya Kweli-4 limeanza kwa jina la msimbo la Yaa Zahra (AS) kwa mashambulizi mseto ya makombora, ndege za kivita zisizo na rubani na operesheni maalumu ya kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya kambi za jeshi la Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Maeneo kumi muhimu na ya kistratijia ya uongozi na zana za kivita za jeshi la kigaidi la Marekani katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Sheikh Isa nchini Bahrain yamepigwa kwa mashambulizi mazito ya vikosi vya ulinzi vya Iran.  

Kituo cha Uongozi na Udhibiti cha Jeshi gaidi la Marekani, maghala ya mafuta na majengo ya makamanda wa ngazi za juu wa Kimarekani katika kambi hiyo ni miongoni mwa shabaha zilizopigwa na kusambaratishwa.

Ripoti za kijasusi na picha za satalaiti zinaonyesha kuwa, miundombinu ya kambi hiyo imeharibiwa kikamilifu na kwamba kunashuhudiwa mgogoro mkubwa wa binadamu na kukimbia kwa magaidi wa Kimarekani kutoka kwenye kambi hiyo.   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *