
George Galloway, mbunge wa zamani wa Uingereza amesema mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Marekani dhidi ya wasichana 167 waliokuwa na umri wa kati ya miaka 7 na 12 wakiwa madarasani katika Shule ya Msingi ya Minab nchini Iran ndio maafa makubwa zaidi yaliyowahi kufanywa na Marekani tangu wakati wa Vita vya Vietnam.
Galloway amesema, katika siku hiyo hiyo ya kwanza ya vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, Jumamosi tarehe 28 Februari, Marekani na Israel ziliua wachezaji 40 wa voliboli, timu tatu kamili za wachezaji wasichana, katika shambulizi la anga nchini Iran.
“Huenda hauna habari ya mauaji ya halaiki ya wanafunzi wasichana nchini Iran. Haya ni mauaji makubwa zaidi ya wasichana katika shule moja ambayo yamewahi kusajiliwa katika historia,” amesema George Galloway.
Mbunge huyo wa zamani wa Uingereza anasema: Jaribu kutafakari, kama Russia ingeua wasichana 167 wakiwa shuleni; lau Iran ingeua wanafunzi 167 katika shule moja, hapana shaka kwamba hiyo ingekuwa habari kubwa zaidi ya vyombo vya habari duniani.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa mazishi ya wanafunzi hao wa kike wa shule ya msingi huko Minab, kusini mwa Iran, yamefanyika leo kwa huzuni kubwa na majonzi, huku wazazi waliokuwa wakiomboleza wapendwa wao wakitoa wito wa kulipiza kisasi dhidi ya mauaji hayo.
Habari hii inaambatana na video ya George Galloway akizungumzia maafa hayo.