Kundi la Wachungaji kutoka mrengo wa kihafidhina wa kanisa Anglikana wanakutana wiki hii mjini Abuja Nigeria, kuchagua kiongozi mbadala wa kanisa hilo tofauti na Sarah Mullally, ambaye amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuongoza kanisa hilo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mullally, anatarajiwa kusimikwa rasmi kama askofu wa Cantebury baadae mwezi huu, na uteuzi wake kama mwanamke wa Kwanza kuongoza kanisa hilo, uliibua hisia mseto wa mawazo, hasa kutoka kwa waumini wa kikristo wenye msimamo wa kihafidhina ambao wanapinga wanawake kuhudumu kama maaskofu.

Kongamano la siku nne la mjini Abuja, limeandaliwa na vuguvugu linalofahamika kama GAFCON, ambapo liliundwa mwaka 2008 kufuatia tofauti za kitheolojia, ikiwemo kuhusu ufungishaji w andoa za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Vuguvugu hili kwa sehemu kubwa limevutia wachungaji na waumini wengi waliogawanyika kutoka barani Afrika, ambapo baadhi wanaunga mkono uteuzi wa Mullally.

Muungano huu wa maaskofu kutoka Afrika, umekuwa katika mvutano hata na mtangulizi wa Mullally, askofu Justin Welby, ambaye alikuwa anaunga mkono ndoa za mashoga.

Ushirika wa Anglikana, dhehebu la tatu la kikristo kwa ukubwa duniani baada ya kanisa Katoliki na Orthodox ya Mashariki, linaundwa na majimbo 42 katika nchi 165, viongozi wake wakisema wanabaki kuwa familia ya makanisa yanayojitegemea lakini yanayotegemeana, licha ya kuongezeka kwa mvutano kuhusu theolojia na utawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *