Nchini Rwanda, Victoire Ingabire na wawakilishi wake wamewasilisha rufaa siku ya Jumatano Machi 4, 2026, dhidi ya kukamatwa kwake mnamo mwezi Juni 2025. Yuko kizuizini kwa karibu miezi minane.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu nchini Rwanda imechunguza rufaa ya Victoire Ingabire siku ya Jumatano, Machi 4, 2026, dhidi ya kukamatwa kwake mnamo mwezi Juni 2025, anaripoti mwandishi wetu huko Kigali, Lucie Mouillaud. Kiongozi huyo wa upinzani alikamatwa kufuatia wito wa kutoa ushahidi katika kesi ya baadhi ya wafuasi wake.

Akiwa kizuizini kwa muda tangu wakati huo, na akikabiliwa na mashtaka ikiwemo “njama ya kuchochea uasi,” Victoire Ingabire analaani uvunjaji wa katiba wa kifungu maalum cha sheria.

Kifungu cha 106 cha sheria inayosimamia taratibu za jinai, ambacho kilisababisha kukamatwa kwa Victoire Ingabire, kinaidhinisha mahakama kuwaita watu wanaochukuliwa kuwa washirika wa washtakiwa kwenye kesi, na kuagiza uchunguzi ufanyike ikiwa maelezo yao hayatoshi.

Mahakama Kuu kutoa uamuzi Machi 27

Hatua hii inakiuka baadhi ya kanuni za kikatiba, kulingana na mawakili wa kiongozi wa upinzani, haswa dhana ya kutokuwa na hatia na mgawanyo wa mamlaka ya mahakama. Upande wa utetezi unasema kwamba uchunguzi wa ufunguzi wa amri za mahakama unaathiri uhuru wa uchunguzi na kazi ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma.

Hoja hizi zinakataliwa na wakili wa serikali: kifungu cha sheria kinaipa mahakama mamlaka ya kuhakikisha kwamba kila mtu anawajibika kwa matendo yake, anabainisha, na ufunguzi wa uchunguzi haimaanishi kwamba mashtaka yatawasilishwa. Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi Machi 27.

Kiongozi mkuu wa upinzani na mkosoaji wa rais Paul Kagame, Victoire Ingabire alirudi kutoka uhamishoni mwaka 2010 kugombea urais. Alikamatwa mwaka huo huo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mwaka 2013 kwa mashtaka yanayohusiana na usalama wa taiafa na kupinga mauaji ya kimbari ya Watutsi; mashtaka ambayo amekuwa akiyakanusha kila wakati. Aliachiliwa huru mwaka wa 2018 kufuatia msamaha wa rais, lakini alikataliwa kuondoka nchini na hakupata tena haki zake zote za kiraia—ikiwa ni pamoja na haki ya kugombea wadhifa—na chama chake cha upinzani hakijatambuliwa rasmi. Mnamo mwaka 2025, alikamatwa tena na kushtakiwa kwa madai ya kuhusika katika kundi la wahalifu na kuchochea machafuko ya umma, madai ambayo anakanusha. Kesi yake hutajwa mara kwa mara na mashirika yasiyo ya kiserikali na waangalizi wa kimataifa kama mfano wa vikwazo vikali kwa upinzani wa kisiasa nchini Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *