
Saa chache baada ya barua ya kujiuzulu ya Thomas Boni Yayi, iliyoandikwa siku ya Jumatano, Machi 3, 2026, maafisa wakuu wa chama cha upinzani cha Les Démocrates wameitisha mkutano wa kamati ya kudumu katika makao makuu ya chama huko Cotonou. Mkuu huyo wa zamani wa nchi alituma barua kwa sekretarieti ya utawala ya chama hicho akitangaza kujiuzulu kweye nafasi ya kiongozi wa chama, akitaja sababu za kiafya. Chama bado hakijakubali rasmi kuondoka kwake na kinakusudia kukutana naye kwanza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan
Maafisa wote muhimu wa chama walikuwepo siku ya Jumatano, Machi 4, 2026, katika makao makuu ya chama cha Les Démocrates kwa mkutano uliodumu zaidi ya saa moja. Kwenye ajenda: barua ya kujiuzulu ya kiongozi wao wa muda mrefu, rais wa zamani Thomas Boni Yayi.
Kufuatia mkutano huo, uongozi bado haujathibitisha kuondoka kwa rais huyo wa zamani, kama ilivyoelezwa na katibu wa mawasiliano, Guy Mitokpè. “Kwa sasa, chama hakiwezi kuzungumzia chochote kuhusu barua hii,” alisema. “Hili linamhusu kiongozi muhimu zaidi katika chama cha Les Démocrates. Kwa hivyo, hatuwezi kusema, kwa sasa, kwamba tunalikubali. Ni muhimu kwamba ujumbe uweze kukutana naye na kujadili jambo hilo.”
Mkutano na Boni Yayi kabla ya Ijumaa?
Kamati ya kudumu inataka mazungumzo ya moja kwa moja na kiongozi aliyejiuzulu, labda ili kumshawishi abaki, au kuheshimu uamuzi wake wa kujiuzulu, uamuzi uliotajwa rasmi kwa sababu za kiafya.
Kufikia Jumatano jioni, ujumbe huo ulikuwa bado haujaundwa, lakini wajumbe wa kamati ya kudumu walikusudia kuunda ujumbe huo haraka.
Lengo lao ni kukutana na Boni Yayi kabla ya Ijumaa, Machi 6, tarehe ya mkutano wa kitaifa wa uratibu uliopangwa. Hapo awali, mkutano huu ulikuwa wa kuzingatia msimamo wa chama kuhusu uchaguzi wa rais wa Aprili 12, ambao utamchagua mkuu wa nchi kwa muhula wa miaka saba. Hata hivyo, kujiuzulu kwa Thomas Boni Yayi bila shaka itakuwa mada ya majadiliano katika mkutano huo.