Marekani na Israel, zimeendelea kutekeleza mashambulizi ya angaa kwa wiki ya pili leo nchini Iran, ambayo imekuwa ikilipiza kisasi katika nchi za eneo la Ghuba.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump, ametishia kuwa siku ya Jumamosi, Iran itashuhudia mashmbulizi makubwa huku rais wa nchi hiyo Masoud Pezeshkian, akiapa kuwa nchi yake haitajisalimisha.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Trump amesema, Iran itashambuliwa kwa nguvu siku ya Jumamosi na kusababisha uharibifu mkubwa.

Israel nayo imesema inaendelea na mashambulio makubwa na mazito nchini Iran, kwa kurusha mabomu kwenye chuo cha mafunzo ya kijeshi, kituo cha mawasiliano kilichopo ardhini na kituo cha kuhifadhi makombora na kuendelea kulishambulia kundi la Hezbollah nchini Lebanon.

Vita nchini Israel vinaendelea kwa wiki ya pili sasa na hakuna matumaini kuwa vitamalizika hivi karibuni, huku Marekani ikilenga kushambulia maeneo mapya nchini Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *