Msemaji wa Kamandi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ya Khaatamul-Anbiyaa amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakaribisha na kusubiri kwa hamu kubwa kuthibiti kwa madai ya vikosi vya jeshi la Marekani vya kusindikiza meli za mafuta na kujikita kwenye Lango-Bahari la Hormuz.

Luteni Ebrahim Zulfighar ameeleza hayo kupitia taarifa leo Jumamosi na kubainisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaheshimu maslahi na mamlaka ya taifa ya kujitawala ya majirani zake na hadi sasa haijakiuka mpaka wowote wa mamlaka hayo.

Luteni Zulfighar ameongeza kuwa, sehemu yoyote itakayotumiwa kufanyia uchokozi dhidi ya Iran itakuwa shaba halali ya kulengwa, hakuna kurudi nyuma katu katika kukabiliana na Marekani na utawala wa kizayuni.

Msemaji wa Kamandi ya Khaatamul-Anbiyaa ameendelea kueleza kwamba: “nchi ambazo hazijaipatia mahala na suhula Marekani na utawala wa kizayuni hadi sasa hazijawa mlengwa wetu na kuanzia sasa na kuendelea hazitakuwa hivyo, lakini vituo vyote vitakavyokuwa kianzio cha uchokozi dhidi ya Iran azizi, kama ilivyokuwa hapo kabla zitaandamwa na mashambulizi makala ya nchi kavu, baharini na angani.

Luteni Zulfighar ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakaribisha na kusubiri kwa hamu kubwa kuthibiti kwa madai ya vikosi vya jeshi la Marekani vya kusindikiza meli za mafuta na kujikita kwenye Lango-Bahari la Hormuz…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *