
Mlipuko mkubwa umesikika usiku wa Jumamosi, Machi 7 kuamkia Jumapili, Machi 8, 2026, nje ya ubalozi wa Marekani huko Oslo, Norway, lakini hakuna majeraha yaliyoripotiwa, polisi ya Norway imetangaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mlipuko huo ulitokea karibu saa 7:00 usiku saa za ndani (saa 7:00 saa za Ufaransa), polisi wamesema, wakiongeza kuwa hawakuwa na taarifa katika hatua hii kuhusu chanzo chake. Kulingana na kamanda wa operesheni za polisi Michael Dellemyr, aliyehojiwa na kituo cha habari cha umma NRK, mlipuko huo umeharibu mlango wa kuingia katika sehemu ya ubalozi wa Marekani.
“Uharibifu ni mdogo,” amesema Dellemyr. “Hatutatoa maoni kuhusu aina ya uharibifu, kilicholipuka, au maelezo mengine yanayohusiana na shambulio hilo mbali na taarifa kwamba kulikuwa na mlipuko,” ameongeza, akibainisha kuwa “uchunguzi ndio unaanza.” Idadi kubwa wa maafisa wa polisi imewekwa kuzunguka ubalozi.