Rais wa Marekani, Donald Trump hapo jana baada ya mkutano wa NATO nchini Uturuki, alirejea nyumbani kwa kutumia ndege yake ya zamani ya Air Force One badala ya ile mpya aliyopewa zawadi na nchi ya Qatar, uamuzi aliouchukua saa chache baada ya nchi yake kufanya mashambulizi Iran.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Trump hakueleza bayana ni kwanini aliamua kubadili ndege licha ya kuisifia ndege yake mpya, badala yake alirejea nyumbani kwa kutumia ya zamani akisema ni sababu za kumbukumbu na hakuna uhusiano na mashambulizi yaliyofanywa Iran.

Mabadiliko ya ndege, yameibua maswali mapya kuhusu usalama wa ndege hiyo mpya ambayo Marekani ilitumia dola milioni 400 kuijenga upya.

Picha za ndege mpya zilizopigwa hivi karibuni, zinaonesha kuwa huenda ndege hii haikuwa na vifaa kama ile ya zamani ambayo ina uweze wa kupata ishara kama kuna hatari ya roketi na hatua inazoweza kufanya kama ile ya zamani ili kukwepa hatari.

Rais Trump akiwa kwenye ndege ya Air Force One.
Rais Trump akiwa kwenye ndege ya Air Force One. REUTERS – Jonathan Ernst

Kwa mara ya kwanza Trump alitangaza kupitia mitandao yake ya kijamii kwamba ndege yake mpya imeonekana kupendwa na watu wengi na kwamba itasafiri kwenda Uingereza kwenye moja ya kambi yake kubwa zaidi ya kijeshi ili wanajeshi wake wapate nafasi ya kuiona.

Trump alirejea nyumbani kutoka Uturuki kwa kutumia ndege ya zamani aina ya Boeing VC-25As ambayo imebeba marais kwa zaidi ya miongo mitatu na nusu.

Awali kampuni zinazofuatilia safari za ndege zinaeleza kuwa zilishindwa kubaini mahali iliko, na kwamba huenda marubani walizima vifaa vya rada ya ndege hiyo, mbinu ambayo inatumika wakati inaposafirisha marais.

Donald Trump, akiwa kwenye mkutano wa NATO
Donald Trump, akiwa kwenye mkutano wa NATO REUTERS – Yves Herman

Hata hivyo ndege za viongozi wengine wa NATO zilionekana kwenye rada ikiwemo ile ya Kansela wa Ujerumani na waziri mkuu wa Uingereza.

Ndege mpya aliyozawadiwa na Qatar aina ya Boeing 747-800 na baadae kufanyiwa marekebisho ili kumbeba rais Trump, iliondoka Uturuki majira ya asubuhi siku ya Jumatano na kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa RAF Mildenhall nchini Uingereza, JUmatano mchana, rada za ufuatiliaji zimeonesha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *