Wazazi na walezi wilayani korogwe mkoani Tanga wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika malezi ya watoto kwani baadhi yao wamekuwa ndio chanzo cha watoto kuwa na tabia sisizo pendeza kwenye jamii.
Rai hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la korogwe mji Cpa. Charles Njama katika ibada ya maalumu ya pamoja kuombea wanawake na watoto kwa waumini wa makanisa mablimbali iliyofanyika katika kanisa la kkkt korogwe.
Kwaupande wake,mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mchungaji William Kope amesema kuwa wanawake wengi hapa nchini wanateswa na mfumo dume jambo ambalo limekuwa likiwanyima haki zao za msingi.
Katika hatua nyengine Mbunge njama amewaunga mkono wanawake hao kwa kutoa mahitaji mbalimbali kwaajili ya kusaidia watoto yatima.
(Feed generated with FetchRSS)