
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema wananchi wa Marekani wanapaswa kujua kwamba utawala haramu wa Israel umeiburuta Marekani na kuitumbukiza kwenye vita na Iran.
Ismail Baqaei amesema hayo aliporusha hewani tena ujumbe wa seneta wa Marekani, Chris Murphy kwenye mtandao wa kijamii wa X uliosema: Hili ndilo jambo ambalo watu wa Marekani wanapaswa kulijua.
Baada ya kushiriki katika kikao cha siri cha viongozi wa serikali ya Donald Trump kuhusu vita vya sasa dhidi ya Iran, Seneta wa chama cha Domocratic, Chris Murphy, amekosoa vikali mwelekeo wa sasa wa serikali ya Washington na kusema: Israel imetulazimisha jambo hili, na suala hili linaonesha wazi udhaifu mkubwa wa Marekani kwamba waitifaki wetu wanaweza kutuburuta kwenye vita ambavyo vina madhara kwa maslahi na usalama wetu wa taifa. “Tumekuwa dhaifu kiasi gani?” amesema Seneta Chris Murphy.