Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Elimu Duniani, Gordon Brown, amesema watoto hawapasi kufanywa wahanga wa vita, na shule na hospitali hazipaswi kushambuliwa.

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Uingereza ambaye kwa sasa ni Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Elimu Duniani ameandika kuwa: Watoto hawapasi kuwa wahanga wa vita, na shule na hospitali hazipaswi kushambuliwa.

Gordon Brown ametoa wito wa kuanzishwa mahakama maalumu ya kushughulikia jinai zinazofanywa dhidi ya wanafunzi katika upeo wa kimataifa.

Afisa huyo wa UN pia ametaka kufuatiliwa kisheria wale waliohusika na mauaji ya wanafunzi wa shule ya wasichana ya Minab nchini Iran na kusema: Shambulizi dhidi ya shule ya msingi ya Minab limeonyesha kuwa, shule na wanafunzi sasa zimekuwa shabaha ya mashambulizi.

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ameongeza kuwa, “shule ambazo zinapaswa kuwa kimbilio salama la wanafunzi zimegeuka na kuwa makaburi yao.”  

Tarehe 28 Februari serikali ya Marekani ilikiuka sheria zote za kimataifa na kushambulia shule ya Msingi ya watoto wa kike ya Minab katika mkoa wa Hormuzgan (kusini mwa Iran) ambapo wanafunzi karibu 170 wa kike na walimu 20 wa shule hiyo waliuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *