Watendaji na watumishi wa serikali walio katika ngazi ya maamuzi wamehimizwa kuwa wabunifu katika kutambua fursa za uwekezaji na kushirikisha sekta binafsi katika mpango wa PPP ili kuharakisha maendeleo.

Watendaji wakuu na wakurugenzi kutoka mashirika na taasisi za serikali na sekta binafsi pamoja na maafisa wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na Taasisi za fedha nchini, wameingia siku ya nne ya mafunzo katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) Jijini Dar es salaam.

Mbali na mafunzo ya darasani pia wametembelea miradi kadhaa ya Ubia kati ya serikali na sekta binafsi yaani PPP ambapo wakiwa mradi wa Mlimani, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mlimani Holdings Ltd Pastory Mrosso, amewaeleza umuhimu wa watendaji hao kuishirikisha kikamilifu sekta binafsi kwenye miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkufunzi Mwandamizi Elekezi wa Jeshi la nchi Kavu Kanali Khaji Mtengela, amesema mafunzo hayo mafupi kwa watendaji hao kutoka sekta ya umma na binafsi yamekuwa na tija kubwa katika kuimarisha ubia wa kimkakati katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050.

Washiriki wa mafunzo hayo kupitia kwa
Mkuu wa Idara ya Biashara kubwa Sekta ya Umma Rahma Dachi, amesema yamewaongezea kujiamini na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mafunzo hayo ya kozi fupi ya 17 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania ya siku tano yanatarajiwa kuhitimishwa Ijumaa hii.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *