Kundi moja la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi na jinai zinazofanywa na Marekani na Israel dhidi ya wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Lebanon.

Kwa mujibu wa Devdicourse, wataalamu hao wa UN wamesema operesheni za kijeshi zinazofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Lebanon zinakiuka wazi sheria za kimataifa, na yumkini zikawasha moto mkubwa zaidi wa vita vya kieneo.

Katika taarifa yao, wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema wamesikitishwa na operesheni za kijeshi zinazofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Lebanon, kwani zilianzishwa katikati ya mazungumzo ya kidiplomasia.

Wamesisitiza kuwa, mashambulizi na jinai zinazofanywa na Marekani na Israel dhidi ya wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Lebanon ni haramu na ni sawa na uvamizi.

Wataalamu hao wa haki za binadamu wa UN wamesisitiza kuwa, Marekani na Israel zinapasa kuacha tabia ya kujichukulia hatua zinazokanyaga sheria za kimataifa za haki za binadamu pasi na kuwajibishwa.

Kundi hilo la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa limesema wananchi wa Iran ndio wanaopasa kufanya maamuzi juu ya mustakabali wa nchi yao, huku wakitoa mwito wa kuheshimiwa uhuru na mamlaka ya kujitawala Jamhuri ya Kiislamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *